Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.
Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.
Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.
Kwa
mujibu wa kamanda, mwanamke huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Jenipher
Peter (45). Alisema alikuwa akiishi na mume wake, Peter Mrosso (43)
pamoja na watoto wao watatu. Alisema mwili wake ulifukiwa ndani ya boma
la ng'ombe.