MBUNGE wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), amewasha moto bungeni akifunguka kuwa atawaambia wananchi wake wasiipigie kura CCM pamoja na yeye mwenyewe kama maji hayatapatikana jimboni mwake wakati akichangia katika majiadiliano ya hoja za kamati bungeni leo.
Pia Lugola
amehoji kwa nini nguvu zinazotumika kuwapiga watu kama akina Profesa
Lipumba zisitumike kupambana na wawekezaji wanaokiuka masharti ya
uwekezaji na kuwanyanyasa wananchi huku akimtaka Waziri mpya wa Ardhi,
Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi kushughulikia vilivyo kero za
ardhi.