Wabunge 35 wa kambi ya upinzani bungeni jana walitolewa nje ya
ukumbi wa bunge na spika wa bunge Anne Makinda na kupewa adhabu ya
kutokuhudhuria vikao vitano kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge .
Mara baada ya kikao cha bunge kuanza spika wa bunge alinza kwa
kuwakumbusha wabunge namna ya kufuata kanuni hasa pale wanapotaka
kuondoa muswada wowote.
Hali ilibadilika ghafla Bungeni baada ya Mbunge Ezekiel Wenje kuomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?
Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… ndipo spika aliamua kuwatoa nje.
Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni
ya sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi
pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji
Tanzania iliwasilishwa Bungeni.
Majina ya Wabunge waliotimuliwa ni,
- Ezekiel Wenje
- Mussa Kombo
- Masoud Abdallah Salim
- Rebecca Ngodo
- Sabrina Sungura
- Khatib Said Haji
- Dr. Anthony Mbassa
- Maulidah Anna Valerian Komu
- Kulikoyela Kahigi
- Cecilia Pareso
- Joyce Mukya
- Mariam Msabaha
- Grace Kiwelu
- Israel Natse
- Mustapha Akonaay
- Konchesta Rwamlaza
- Suleiman Bungura
- Rashid Ali Abdallah
- Ali Hamad
- Riziki Juma
- Rukia Kassim Ahmed
- Azza Hamad
- Khatibu Said Haji
- Kombo Khamis Kombo
- Ali Khamis Seif
- Haroub Mohammed Shamisi
- Kuruthum Jumanne
- Mchuchuli
- Amina Mwidau
- Mkiwa Kimwanga
- Salum Baruhani
- Marry Stellah Malaki
- Rashid Ally Omary
- Mwanamrisho Abama
- Lucy Owenya