2015
ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania, kila siku stori za Siasa zimekuwa
kwenye headlines nyingi kuanzia Magazetini, kwenye TV, mitandaoni na Radioni .
Mbunge
James Lembeli alikuwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Mazingira na Maliasili.. kuna habari za baadhi ya Wabunge wametangazwa
kuhama Vyama vyao, Lembeli kathibitisha kuhama CCM kwa maneno yake
mwenyewe.
"Nimetafakari,
nimezungumza na mama yangu kwa zaidi ya saa kumi.. mke wangu na watoto
wangu, na kwa kusikia kilio cha wananchi wa Jimbo la zamani la Kahama
nimeamua kutangaza kuanzia leo kwamba natangaza kujiondoa uanachama
wangu ndani ya CCM" - James Lembeli.
"Nilikipenda
lakini nimelazimika kuchukua uamuzi huu, najua nawakera wengi lakini
nawaomba waangalie hali ambayo Viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama
wamesababisha niamue uamuzi huu mgumu.
"Kuanzia
leo najiunga na CHADEMA… Namshukuru Rais Kikwete, nafikiri atakuwa mtu
wa kwanza kuamini haya ninayosema, mwaka 2010 mizengwe iliyofanyika
lengo lake ilikuwa kukata jina langu, kila mtu anafahamu Rais mwenyewe
aliwahi kuniambia lakini Rais Kikwete ndiye aliyerudisha jina langu…
Ninaahidi nitaendelea kufanya kazi nae mahali popote, na MUNGU naomba
anisaidie niweze kuvuka salama katika haya"- James Lembeli.