WATU wanne wamefariki dunia na wengine 11 wakijeruhiwa katika ajali
ya gari iliyotokea Wilaya ya Hai, Kilimanjaro ikihusisha gari aina ya
Hiace iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Sanya Juu na Moshi baada ya
kugongana na Fuso.
Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence
Ngonyani, amesema ajali hiyo imetokea saa moja asubuhi, ambapo majeruhi
nane wamelazwa katika Hospitali ya Mawenzi na (KCMC) kwa matibabu na
baadhi yao hali zao ni mbaya.