Taarifa
kutoka mkoani Dodoma zinasema watu zaidi ya 10 wamefariki dunia
usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada
ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka
Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na
kisha kupinduka.
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa
katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.