Chama cha TLP kimesema hakipo tayari kuungana na chama kingine chochote kile kwa makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja badala yake kitasimamisha mgombea wake makini ambaye ataingia katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya urais.
Kauli
hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha TLP taifa Dominata
Rwechungura wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kishogo wilayani
Bukoba ambapo amewataka watanzania kuendelea kuwa na imani na chama
hicho huku akiwasisitiza wananchi kutowasikiliza wanasiasa wanaopanda
kwenye majukwaa na kuwarubuni.
Rwechungura
ametoa tahadhari kwa watanzania ili wasikubali kununuliwa kwa gharama
nafuu na wanasiasa wanaopitisha pesa kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa
hali ambayo inaweza kusababisha kupata viongozi wabovu wasio na sifa ya
kuliongoza taifa.
Katika
hatua nyingine naibu katibu mkuu wa TLP Dominata Rwechungura amelaani
vikali juu ya wanasiasa wanao jilimbikizia pesa za walipakodi ambazo
zilitakiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi huku
makamu mwenyekiti wa TLP taifa Bw. Joas Kayura akiwataka watanzania
kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kutochagua viongozi
wabovu badala yake wawe makini na kuchangua viongozi wazalendo wenye
sifa za kuliongoza taifa kwa umakini