CHAMA cha Democratic Party (DP) kimetangaza kwenda mahakamani kukishtaki Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na makada wake sita kutokana na kukiuka sheria ya nchi, taratibu pamoja na kanuni za uchaguzi.
Hayo
yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho
Mchungaji Christopher Mtikila, wakati akizungumza na waandishi wa
habari. Alisema makada hao pamoja na chama chao wamekiuka sheria za nchi
pamoja na kanuni za uchaguzi.
Aliwataja makada ambao atawaburuta mahakamani kuwa ni Mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa pamoja na Frederick Sumaye.
Wengine ni January Makamba, William Ngeleja, Stephen Wassira pamoja na Benard Membe. Alidai makada hao walivunja sheria za nchi pamoja na kanuni za uchaguzi kutokana na kuanza kampeni zao mapema.
Wengine ni January Makamba, William Ngeleja, Stephen Wassira pamoja na Benard Membe. Alidai makada hao walivunja sheria za nchi pamoja na kanuni za uchaguzi kutokana na kuanza kampeni zao mapema.
Alisema
watakishtaki Chama Cha Mapinduzi kutokana na kushindwa kuwachukulia
hatua na kuendelea kuwaweka katika mchakato wa kutafuta mgombea wa urais
wa chama hicho wakati walishavunja sheria pamoja kanuni za uchaguzi,
kwahiyo walitakiwa kukatwa mapema kabisa.
"Watu
wameanza kampeni mapema na kwa kufuata sheria ya nchi taratibu pamoja
na kanuni za uchaguzi ni kwamba watu hao wamevunja Sheria kwa hiyo
tunapeleka kesi mahakamani kuwashtaki wao pamoja na chama chao kwa
kuvunja sheria," alisema Mtikila na kuongeza;
"Tunaenda
mahakamani kuishtaki CCM iliyochezea uhuru wetu kwa miaka 54 pamoja na
hawa watu wao kwani hawafai na hii nchi inapoelekea ni kubaya."
Alisema
uchaguzi wa mwaka huu hautakuwa halali kama sheria hazitafuatwa na
kudai kuwa vitu vinavyounyima uchaguzi wa mwaka huu uhalali ni pamoja na
watu kuvunja sheria kwa kuanza kampeni mapema.
Alisema inashangaza kuona pesa zinatumika bure bila sababu ya msingi na kudai kuwa ni uhalifu mkubwa tena wa kimataifa.
Alisema watu wanaotumia pesa wakiachwa kitatokea kitu kibaya nchini, hii ni mbaya sana kwani pesa zinazotumika kwa sasa lazima ijulikane zinatoka wapi.
Alisema watu wanaotumia pesa wakiachwa kitatokea kitu kibaya nchini, hii ni mbaya sana kwani pesa zinazotumika kwa sasa lazima ijulikane zinatoka wapi.
Alisema fedha hizo zinazotumika ipo siku zitakuja kurudi mahali pake kwa hao watu wanaozitoa.
Aliendelea
kusema kuwa inashangaza kuona watu wanatumia pesa kutafuta urais.
Mtikila alimshukia moja kwa moja Lowassa akisema hastahili kupewa nafasi
hiyo.
"Lowasa hastahili nafasi hiyo na wanasheria wetu wapo katika maandalizi ya kuandaa kesi kwa ajili ya kuwapeleka mahakamani," alisema Mtikila.
Alisema
endapo wataona katika chama chochote kuna vitendo kama ambavyo havifai
hawatasita kufuata utaratibu wa kwenda mahakamani endapo watakuwa na
ushahidi wa kutosha.
Alisema DP ipo kwenye maandalizi na wakati ukifika watu wote watafikishwa mahakamani.
Alisema DP ipo kwenye maandalizi na wakati ukifika watu wote watafikishwa mahakamani.