RAIS Jakaya Kikwete, jana amezindua na kuzitunukia Kamisheni meli mbili za kivita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Wanamaji ambazo zitatumika kufanya doria na kulinda mipaka ya majini katika Bahari ya Hindi.
Meli
hizo zimepewa majina ya P77 Mwitongo na P78 Msoga zenye urefu wa mita
60 na zina uwezo wa kufanya doria katika kina kirefu cha maji.
Rais
Kikwete alisema, kupatikana kwa meli hizo kumeifanya Tanzania kuandika
ukurasa mpya wa uhusiano kati yake na China ambao uliasisiwa na waasisi
wa mataifa hayo hayati Mwalimu Nyerere na Mao Tse Tung.
Alisema
meli hizo zimekuja nchini kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China
zikiwa na uwezo wa kubeba silaha nzito kila moja ikiwa na mizinga miwili
mikubwa na midogo sita.
"Jeshi
letu la Wanamaji wakati linaanzishwa 1971, lilisaidiwa na Serikali ya
China meli 13, rada na wataalamu wetu kupatiwa nafasi mbalimbali za
mafunzo...meli hizi zitatuongezea ulinzi katika mipaka yetu majini.
"Kilio
kikubwa cha jeshi letu kilikuwa uwezo mdogo wa meli zetu, tumekuwa na
kazi ya kutafuta meli hizo na sasa tuna mpango wa kuchukua meli nyingine
kubwa zaidi zenye uwezo, kilichobaki ni taratibu za kifedha tu," alisema Rais Kikwete.
Aliongeza
kuwa, lazima Tanzania ijenge uwezo wa kulinda mali zetu, mipaka, samaki
na mitambo ya gesi ambayo imesimikwa baharini hivi karibuni.
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussen Mwinyi, alisema Serikali ya China imekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua
rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo
kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini
Dar es salaam jana April 28, 2015
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na
makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS
Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni
jijini Dar es salaam jana April 28, 2015Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema jeshi hilo
limepiga hatua katika ununuzi wa dhana za kivita na kuendeleza mafunzo
ya kijeshi.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward
Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika
Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili
za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe
zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam jana April 28, 2015.
(PICHA NA IKULU)