NAFDA

NAMFUA FLAG DEVELOPMENT ASSOCIATION.

Friday, July 17, 2015

MAJONZI: Tasnia ya mziki yappata pigo tena....Mwanamuziki Banza Stone Afariki Dunia


Muimbaji wa muziki wa dansi aliyewahi kutamba akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta na TOT Band, Ramadhan Masanja maarufu kama Banza Stone amefariki dunia mchana wa Ijumaa, July 17.
 

Banza alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Taarifa kuhusu kifo chake zimethibitishwa na kaka yake pamoja na mmiliki wa Twanga Pepeta, Asha Baraka. 
 
Kwa mujibu wa kaka yake, Jabir Masanja, msanii huyo alikuwa anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa alizokuwa anatumia zilikuwa kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.
 
Hivi karibuni mama yake mzazi aliongea na kituo cha redio cha EFM na kukiambia kuwa afya ya mwanae ilizidi kuzorota na alianza kugoma kula chakula wala kunywa kunywa dawa. Mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo. 
 
Aliongeza kuwa pamoja na kuugua hivyo bado wasanii wenzake walishindwa kwenda kumjulia hali.
 
“Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.
 
Kabla ya hapo muimbaji huyo alizushiwa kufariki mara nyingi. Wiki chache zilizopita Banza alimongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM kukanusha.
 
“Ndio naumwa kichwa kina nisumbua sana lakini sasa hivi naendelea vizuri yaani hizo habari za kuzushiwa kifo naona sasa hivi kwangu sijui hata itakuwa mara ya ngapi, maana nimeshazushiwa sana. Mimi mzima na huyo anayeeneza azunguke na mikoa mingine aeneze vizuri,” alisema Banza.
 
“Lakini mimi nipo nyumbani hapa Sinza kwa Mama yangu sasa hivi hapa napata juice yaani marehumu anaongea,” aliongeza Banza kwa kicheko.
 
“Inshallah nikiwa vizuri mashabiki wangu wataniona tu lakini nipo mzima.”
 
Msiba upo nyumbani kwao Sinza, Dar es Salaam. Kwa wale wanaopenda kuchangia msiba wake wanaweza kumchangia kwa kutumia namba: 0715407088 au 0753786016. Maziko ya mwanamziki huyo nguli yatafanyika leo jumamosi ya tarehe 18/07/2015 majira ya saa kumi alasiri 
 
Tulikupenda lakini mungu amekupenda zaidi, jina lake lihimidiwe amen

 
Mungu ailaze mahali pema peponi. Amen.

PICHA: Ajali Mbaya ya Fuso na Hiace Yaua Watu Wanne na Kujeruhi 11.


WATU wanne wamefariki dunia na wengine 11 wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Hai, Kilimanjaro ikihusisha gari aina ya Hiace iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Sanya Juu na Moshi baada ya kugongana na Fuso.

Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, amesema ajali hiyo imetokea saa moja asubuhi, ambapo majeruhi nane wamelazwa katika Hospitali ya Mawenzi na (KCMC) kwa matibabu na baadhi yao hali zao ni mbaya.


Jinsi ya Kuandaa na Kutayarisha Dawa Lishe ya Kunenepesha,Kurutubisha na Kuongeza Mwili


Dawa-lishe  ya  kuongeza, kurutubisha  na  kunenepesha  mwili, ni  dawa  maalumu  kwa  watu  wenye  uzito  wa  chini  (  Under weight ) ambao  wanataka  kuongeza  mwili  na  uzito.


Dawa  hii  huwasaidia  watu  ambao  miili  yao  imedhoofu  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile  kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali.

Na  kwa  wale  watu  wembamba  ambao  wanataka  kuongeza  miili  yao, dawa  hii  huwasaidia  vizuri  sana.

FAHAMU  JINSI NA  NAMNA  YA  KUANDAA NA  KUTAYARISHA   DAWA-LISHE  MAALUMU   YA  KUONGEZA, KURUTUBISHA  NA  KUNENEPESHA  MWILI.

MAHITAJI   YA  DAWA –LISHE

i.           Dawa –lishe vijiko  viwili vikubwa.

ii.         Asali  ya  tende  vijiko  vitano  vikubwa.

iii.       Tangawizi  ya  unga  vijiko  vikubwa  viwili

iv.       Unga  wa ufuta

v.         Maziwa  fresh nusu  lita

vi.       Maji  ya  moto  kiasi  cha  milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills  )


MATAYARISHO
i. Chukua  vijiko  vinne  vyenye  dawa  lishe  yako  kisha  chemsha  na  nusu  lita  ya  maji  hadi  mchanganyiko  wako  utokote  halafu  ipua, chuja , makapi  weka  pembeni  kisha  hifadhi  juisi  yako.

ii.Tayarisha  uji kwa  kutumia  unga  wa  ufuta  na maziwa  fresh

iii.Chukua  vijiko  viwili  vikubwa  vya tangawizi  ya  unga  kisha  changanya  kwenye  kikombe  cha  maji  ya  moto  chenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  hamsini  (  250  mills )

MATUMIZI:
i. Tumia  kunywa  nusu  lita  ya  dawa –lishe  yako  kisha

ii.Tumia kula  vijiko  vinne  vikubwa  vya  asali  ya  tende

iii.Kisha tumia  kunywa  vikombe  vinne  vya  uji  wa  ufuta  ulio changanywa  na  maziwa  fresh

iv.Halafu  kunywa  glasi  moja  ya  moto  iliyo  changanywa  na  vijiko  viwili  vikubwa vya tangawizi  ya  unga.

UTAFANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  MFULULIZO.

Baada  ya  siku  thelathini, utaangalia  na  kujitathmini  kiasi  ulicho  ongezeka. Kama  utataka  kuendelea  kuongezeka  zaidi, utaendelea  kutumia  dozi  hii  hadi hapo utakapo fikia kiwango  utakacho  rizika  nacho.

BEI  YA  DAWA-LISHE : Bei  ya  Dawa-Lishe  ni  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU (TSHS.50,000/=)

JINSI  YA  KUIPATA  DAWA  LISHE:
Dawa  hii  inapatikana  katiuka  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAN  katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  karibu  na  SHULE  YA  SEKONDARI  YA  MT. ANNUARITE.

Unaweza  kufika  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu  AU  unaweza  kuletewa  mahali popote  ulipo  jijini  Dar   Es  salaam.

Kwa  wakaazi  wa  ZANZIBAR  watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti  na  kwa  wateja  wetu  wa  ughaibuni watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Kwa  mawasiliano  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu

0766  53  83   84

Vile  vile  tunayo  dawa  ya  asili  iitwayo  JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME  pamoja  na  jinsi  dawa  ya  JIKO  inavyo  fanya  kazi  tafadhali  tembelea:

Thursday, July 16, 2015

Mhindi Aliyekamatwa na Milioni 700 Dodoma Arudishiwa Fedha zake


Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekanusha taarifa zilizozagaa kuhusiana na Raia wa Asia kukamtwa na fedha zaidi ya sh. m.700 kwa madai ya kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM ili wamchague mmoja kati ya waliokuwa wanawania nafasi ya Urais

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari na kamanda wa polisi mkoani hapa, David Misime mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Amit Kevalramani aliyekamatwa juma lililopita kwenye hoteli ya St Gaspar mjini hapa ni mganyabiashara wa mazao ya nafaka ni siyo mpambe wa wanachama wa CCM waliokuwa wanawania Urais.

Misime amesema mnamo siku ya Julai 11 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi kuna baadhi ya wananchi walitoa taarifa kwa jeshi la polisi kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa katika hotel ya St Gaspar.

“Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli, askari walithibitisha kuwa ni kweli, walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina la Amit Kevalramani (31), Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha sh. 722 milion ambacho alipohojiwa alisema kuwa Julai 10 mwaka huu alifika Dodoma kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya nafaka” amesema Misime na kuongeza;
 
“Alipofika Dodoma hiyo siku majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na kesho yake Julai 12 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu.”

Misime alisema kuwa akiwa katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli hiyo ya St. Gaspar walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa polisi.

Alisema mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa na mchakato wa uchaguzi kati ya makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho.

Alibainisha kuwa uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi umebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.

Aidha imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake.

Wakati huo huo kamanda amesema kuwa mnamo Julai 10 mwaka huu majira ya saa 21:00 eneo la Railway Dodoma jeshi la polisi lilifanikiwa kuwakamata:-

1. HERERIMANA METHODE, MIAKA 21.
2. HATUNGIMANA ALEXIS, MIAKA 20.
3. NIYONGABO JUSTIN, MIAKA 20.
4. NTETURUYE ONESPHORE MIAKA 21.
5. BIKORIMANA LEVIS, MIAKA 21 wote ni Wakazi wa Mabanda Burundi kwa kosa la kuingia nchini na kuishi nchini bila kibali.

Watuhumiwa hawa walikuwa wanasafiri na treni kuelekea Dar es Salaam na walipofika Dodoma Askari wanaosindikiza treni waliwashtukia na walipowakamata na kuwahoji walijieleza kuwa ni raia wa Burundi.

Tunaomba ushirikiano wa wananchi pale wanapoona watu ambao siyo raia wasiwakaribishe bali watoe taarifa kwa vyombo vya dola waweze kuhojiwa kwani hata kama waliingia Nchini na kuhifadhiwa katika makambi yaliyopo Nchini hawaruhusiwi kutoka kwenda mbali na kambi zao bila kuwa na kibali maalum.

Wakenya kumpokea Obama wakiwa uchi ?


Kundi la Wakenya, limejiapiza kumkaribisha rais wa Marekani, Barack Obama, nchini kwao wakiwa hawajavaa nguo ili kuonesha kuwa hawajakubaliana na kitendo cha kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.
 
Obama anatarajiwa kutembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu kuwa rais na kutegemea kuwa na mkutano na wafanyabiashara kuanzia Julai 24-26 mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa barua iliyosambazwa na kundi hilo la wakenya, imedai kuwa watafanya maandamano ya amani jijini Nairobi, Julai 22 na 23 mwaka huu kuanzia Uhuru kona.
 
Wamedai kuwa maandamano hayo yatafanywa na wanawake pia wanaume takriban 5,000 wakiwa watupu bila nguo yoyote kupinga Umoja wa nchi za Amerika kupitisha sheria ya mashoga kutambuliwa kisheria.
 
Wamesema lengo kuu la maandamano wakiwa uchi ni kumuonesha na kuelewesha rais Obama, utofauti uliopo kati ya wanawake na wanaume.
 
Wiki iliyopita, Wakenya hao walienda katika mitaa kuandamana wakimuonya rais Obama, kutothubutu kuzungumzia suala la haki za mashoga kwenye ziara yake ya kutembelea nchi hiyo.
 
Mbunge Charles Njagagua, pia aliwataka wabunge kumfukuza Obama, nje ya Bunge mara moja akigusia haki za mashoga.
 
Naye Makamu wa rais nchini Kenya, William Ruto, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wananchi wake kuwa wamesikia kuwa Marekani wameruhusu uhusiano wa mashoga na mambo mengine yasiyo na maadili na kuwataka viongozi wa dini kutetea nchi yao na kusimamia imani ya nchi yao.

Sunday, July 12, 2015

Nafasi ya Urais CCM........Magufuli Apata Ushindi wa Kishindo



Chama  cha  mapinduzi, CCM kimemteua  Dr .Magufuli  kuwa  mgombea  wa  Urais  2015.

Uteuzi wa  Dr. Magufuli  umetokana na  ushindi  wa  kishindo  alioupata  baada  ya  mkutano  mkuu  kukutana jana   usiku  kwa  ajili  ya  kupiga  kura  ili  kupata  jina moja  kati  ya  matatu  yaliyokuwa  yamependekezwa  na  Halmashauri  kuu  ya  CCM.
 Matokeo  ni  kama  ifuatavyo
1.Magufuli.....87%
2. Amina.......10%
3.Migiro......3%

Thursday, July 9, 2015

Dewji Atangaza Kutogombea Tena Ubunge Singida Mjini


Mbunge wa Singida Mjini (CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amewaliza baadhi ya wapigakura wake wakati akitangaza kutogombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa ya madai ya kubanwa na majukumu ya kifamilia na biashara. 
 
Dewji ambaye amekuwa mwakilishi wa jimbo hilo kwa awamu tatu mfululizo, alitangaza uamuzi wake huo kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.
 
Alisema kuwa aliomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa Singida Mjini mwaka 2000, hakuwa na familia na pia biashara zake hazikuwa kubwa kama ilivyo sasa.
 
Alisema katika kipindi chote cha uwakilishi wake, wakazi wa Singida Mjini wamempa heshima kubwa, ukarimu wa hali ya juu, wema uliotukuka na uvumilivu usio na kifani na kwa hali hiyo, hatawasahau kamwe na ataendelea kuwatumikia kupitia mfuko maalumu aliouanzisha.
 
Aliwataka wakazi hao kuendeleza moto wa maendeleo waliouwasha miaka 10 iliyopita kwa miaka mingine kama hiyo ijayo ili jimbo hilo lipige hatua zaidi.
 
“Kwa kutambua heshima mliyonipa na imani kubwa mliyonionyesha kwa vipindi vyote vya uongozi wangu, ingawa nina huzuni lakini sina budi niwaombe kuwa mwaka huu wa uchaguzi sigombei tena na ninatoa fursa kwa kada mwingine wa CCM anipokee kijiti hiki kuliongoza jimbo letu,” alisema kwa huzuni. 
 
Baada ya kutamka maneno hayo, wananchi wengi katika walipiga kelele kwa nguvu wakionyesha kutokubaliana na uamuzi wake. Huku moja ya sauti ikisikika... “Hatutaki mbunge mwingine ni wewe tu hadi tukuchoke.”
 
Awali, Dewji alitaja baadhi ya maendeleo yaliyofanyika katika vipindi vyake, kuwa ni pamoja na kujenga shule 15 za sekondari kutoka mbili zilizokuwapo.
 
Alisema kwa kutumia fedha zake alijenga na kuchimba visima 45 vya majisafi na salama.