NAFDA

NAMFUA FLAG DEVELOPMENT ASSOCIATION.

Friday, August 21, 2015

JE NI WAJIBU MWANAMKE KUMTUNZA MWANAUME KISHERIA?.
Na  Bashir  Yakub.
Kisheria  ndoa inapokuwa  imefungwa   kuna  haki  za  msingi  ambazo  huibuka.  Hizi  huitwa  haki  za  moja  kwa  moja  ( automatic  right). Huitwa  haki  za  moja  kwa  moja   kwakuwa   hazina  uhiari  katika  kutekelezwa  kwake.  Kuwapo  kwa  ndoa  ndio  kuwapo  kwake  na  hivyo  haihitaji  mtu  kuziomba. Kimsingi  haki  hizi  zipo  nyingi  ambapo  tutaona  baadhi  yake hapa   huku  makala  yakijikita  katika   haki  moja ya  matunzo  kwa  wanandoa.

1.BAADHI  YA  HAKI  ZINAZOIBULIWA  NA  NDOA.
( a ) Haki  ya  tendo  la  ndoa.  Hii  ni  haki  ya  lazima  kwa  wanandoa  na  kutokuwepo  kwake  kunaweza  kubatilisha  ndoa iwapo  mmoja  wa  wanandoa ataamua  kufanya  hivyo. Ni  haki  ambayo  huchukuliwa  kama  ndio ndoa yenyewe  na  hivyo  kuifanya  kuwa  na  umuhimu wa pekee.

( b ) Haki  ya  kutumia  jina la mume. Hii   ni haki  aliyonayo  mwanamke  ambapo  anaruhusiwa kutumia  jina  la  mme  wake  badala  ya  lile  la  baba  yake. Hata  hivyo  sheria  haikueleza  iwapo  mwanaume  naye  anaweza  kutumia  jina  la  mke  wake,  au  la  baba  wa  mke  wake, au la  ukoo  wa  mke  wake.  Pia si  tu  mwanamke  ameruhusiwa  kutumia  jina  la  mme  wake  isipokuwa  hata  lile  la  ukoo  wa  mme  wake.

( c ) Haki  ya  kutumia  mali  za  familia  kwa  pamoja. Haijalishi  mali  hizo  ni  mwanamke  mwanaume  ataruhusiwa  kutumia na  haijalishi  mali  hizo ni  za  mwanaume  mwanamke  ataruhusiwa  kutumia. Isipokuwa  yawe  matumizi  ambayo  hayako  kinyume  cha  sheria.

( d ) Haki  ya  kutunza  watoto/mtoto kama  yupo. Ikiwa  familia  imebarikiwa  na  mtoto/watoto basi  wanadoa  kwa  pamoja  wanawajibika  kuwatunza  watoto  hao  kila  mtu kwa  nafasi  yake. Hii  ina  maana mwanamke  anawajibika  zaidi  kuwa  mwangalizi  mkuu wa  kila  siku  wa  watoto  huku  mwanaume  akilazimika  kutoa  matumizi   hasa  yale ya  kifedha.

( e ) Haki  ya  kugawana  mali  pindi  ndoa  inapovunjika. Hii  huhusisha  mali    zote  ambazo  huitwa  mali  za  machumo  ya  pamoja  baina  ya  mwanamke na  mwanaume.

( f ) Pia  ipo  haki  ya  kurithi  na  kurithiana  iwapo  kuna  kifo  cha  mmoja  wa  wanandoa. Mwanamke  aweza  kurithi  mali  za  mme  wake  halikadhalika  mwanaume. Hii  huenda  mpaka  kwa  watoto  waliopatikana  katika  ndoa  ambapo   huweza  kurithi  mali  za  baba, mama  au  wote  wawili.

( g ) Haki  ya  matunzo  baina  ya  wanandoa.  Hii  ndiyo  itakayojadiliwa  japo  kwa  ufupi .

2.  MWANAUME  KUMTUNZA  MWANAMKE.
Sura  ya  29  ya  Sheria  ya  ndoa  kifungu  cha  63 ( a )  kinasema  kuwa  ni  wajibu  wa  kila  mwanaume  kumtumza  mke/wake zake  kutokana  na  njia  za  kipato  chake.  Neno  njia  za kipato  chake  maana  yake  ni  namna  anavyopata   kipato  ndivyo  atavyotakiwa  kutoa  matunzo  kwa  mwanamke.  Haiwi  kuwa  mwanaume  anapata  kipato  kidogo  halafu  alazimishwe  kutoa   matunzo  makubwa.  Ushahidi  wa  namna  anavyopata  kipato  chake  ndio  utakaoainisha  kiasi  cha  matunzo  kwa  mke  wake.

Aidha kwa  mujibu  wa  kifungu  hicho  matunzo  yanayoongelewa  hapa  yanahusisha   makazi,  mavazi, chakula  na  huduma  nyingine  kama  za afya  n.k. Kitu  cha  msingi  hapa  ni  kuwa  ni  lazima  kwa  mwanaume  kutoa  vitu  hivi  kwa mke  wake.

3.  MWANAMKE  KUMTUNZA  MWANAUME.
Kifungu  hichohicho  cha  63 ( b ) kinasema  kuwa  utakuwa  ni  wajibu  wa  kila  mwanamke  lakini  mwenye  uwezo  kutoa  matunzo  kwa   mume  wake  iwapo  mume  huyo  ana  ulemavu/hajiwezi  jumla  au  sehemu  ya  mwili  wake, kiakili  au  kimwili  na  hivyo  kutokuwa  na  uwezo  wa  kuingiza  kipato  kutokana  na  hali  hiyo.

Kwa  kifungu  hiki  tunaona  kuwa mwanamke  anao  wajibu  wa  kumtunza  mume  wake   lakini  iwapo  tu kwanza  ana  uwezo, pili mwanaume  awe  na  tatizo  ambalo  kwalo  hawezi  kuingiza  kipato  na  tatizo  hilo  liwe la  kimwili  au  kiakili. Kumbe  basi  tunaona  kuwa mwanaume  kumhudumia  mwanamke ni  lazima  hata  mwanamke  awe  mzima  wa  afya  huku   hafanyi  kazi  wakati  mwanamke  kumhudumia  mwanaume  ni  pale  tu  atapokuwa  ana  tatizo  ambalo  linamfanya  asiweze  kufanya  kazi. Lakini  pia  sheria  imesema  mwanamke  atatoa  huduma  iwapo  ana  uwezo wakati  neno  iwapo  ana  uwezo  haikuliwekwa  kwa  mwanaume.Kwa mwanaume  kutoa  ni  kutoa  tu.

MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

Thursday, August 20, 2015


KILA ALIYEJIANDIKISHA ANA WAJIBU WA KUPIGA KURA

Jaji Mstaafu, Damian Lubuva.
Kwanza nimshukuru Mungu kwa kuweza kutupa uhai leo na kujiona tuko katika nchi yetu iliyojaa amani.
Naamini kwamba katika maeneo yote ya nchi, wazalendo wa nchi hii walijitokeza bila kulazimishwa kwenda kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (BVR)kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Mkoa wa mwisho kuhitimisha rasmi kazi hiyo iliyoanza kwa kusuasua mwanzoni mwa mwaka huu ni Jiji la Dar es Salaam.Kabla ya uandikishaji, tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilikuwa imekadiria kwamba mwaka huu kutakuwa na watu milioni 24 wenye sifa za kujiandikisha na hatimaye kushiriki katika uchaguzi huo wa kuwachagua madiwani, wabunge na rais.
Kwa dalili zinavyojionesha, idadi hiyo ya watu milioni 24 inaweza isifikiwe kwa sababu ya matatizo yaliyojitokeza wakati wa uandikishaji ambayo yaliwakatisha tamaa baadhi ya watu kutokana na usumbufu uliokuwepo.
Hata hivyo, kama idadi hiyo itakaribiwa, itakuwa si haba na jambo muhimu baada ya hapo ni waliojiandikisha kuhakikisha kila mmoja anapiga kura. Unapopiga kura ndipo unapoonesha uzalendo wako, kwani unasababisha kupatikana kwa kiongozi bora, usipopiga kura elewa kwamba unachangia kwa kiwango cha juu kusimika viongozi wasiofaa katika nchi hii yenye changamoto nyingi za maendeleo.
Nimesema hivyo kwa sababu kumeanza kutokea tatizo la watu kutotaka kupiga kura na badala yake kutumia zoezi la uandikishaji kupata vitambulisho tu, yaani ile kadi ya mpiga kura kugeuzwa kitambulisho.
Nilisikitika sana kuona katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, zaidi ya nusu ya waliojiandikisha kupiga kura hawakupiga kura, hii ilinisikitisha sana na kwa kweli yule ambaye hakupiga kura ajiambie katika nafsi yake kwamba hakuitendea haki nchi yetu.
Hili ni tatizo kwa sababu kila aliyejiandikisha anatakiwa kupiga kura. Kutopiga kura maana yake ni kuacha masuala muhimu ya nchi yaamuliwe na wachache badala ya walio wengi na ambao hawakupiga kura wakati walikuwa wamejiandikisha mwaka 2010 wajue kwamba walichangia kupata viongozi wabovu katika nchi hii.
Najua kwamba zoezi la uandikishaji wapiga kura ulikuwa na kasoro nyingi na za kukera kwa wananchi waliojitokeza. Baadhi ya matatizo hayo yalikuwa ya kujirudia kiasi kwamba wengine walianza kuhoji kama wahusika wanajifunza kutokana na mwenendo wa mchakato mzima wa uandikishaji.
Naamini kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Mstaafu, Damian Lubuva na serikali kwa ujumla itakuwa imejifunza kutokana na mchakato huu na taifa litajiepusha na mkanganyiko kama huu kwenye chaguzi zijazo.
Binafsi nitafurahi kuona idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura wanafanya hivyo. Tunajua kuwa katika chaguzi nyingi duniani, si rahisi kwa watu wote waliojiandikisha kupiga kura wapate fursa ya kupiga kwa sababu tofauti.
Lakini, kama tunavyoona kwa jirani zetu wa Kenya, tunaweza walau kupata wapiga kura waliofika asilimia 75 ya waliojiandikisha.
Katika baadhi ya nchi za wenzetu, wako wananchi ambao husafiri kutoka Ulaya na Marekani kwa lengo la kuwahi kupiga kura nchini mwao, huo ni uzalendo ambao nasi tunatakiwa kuujenga.Watanzania hawawezi kuacha kupiga kura kwa sababu yoyote ile. Kama unataka kiongozi unayemtaka ashinde katika uchaguzi, unatakiwa kupiga kura.
Watu wengi wakipiga kura, hata uongozi unaoingia madarakani unakuwa na amani kwa vile unafahamu umeingia kwa mamlaka ya walio wengi. Ndani ya moyo wako weka dhamira kwamba ‘uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni lazima nipige kura’, vinginevyo wote watakaoacha kupiga kura wataonekana ni wasaliti wa nchi yao wasio wazalendo.
NEC YAWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUTOKUWA NA UPANDE WAKATI WA KUWAELIMISHA WANANCHI KUHUSU UCHAGUZI MKUU UJAO.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada leo jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria mkutanoni .
 Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC leo jijini Dar es salaam wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.
 Wanasekretarieti ya maandalizi ya mkutano NEC na wadau mbalimbali  na baadhi ya waandishi wakifuatilia mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akiteta jambo na mmoja  wa makamishna wa Tume hiyo Prof Amon Chaligha leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa NEC na wadau mbalimbali.
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi na hatua zilizofikiwa hadi sasa leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini.


MWANDISHI WETU -MAELEZO-DAR ES SALAAM

Tume ya Taifa ya uchaguzi  NEC  imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea  ili waweze kufanya maamuzi sahihi  wakati wa uchaguzi Mkuuu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti   wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa uchaguzi na kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa  taasisi za kidini zinaaswa kama walivyo wadau wengine katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhubiri amani na kuendelea kutoa elimu kwa watanzania ili zoezi hili liishe kwa amani na kuwaacha watanzania wakiwa  na umoja na mshikamano licha ya tofauti za kiimani zilizopo miongoni mwao.

“Tume inawataka, nyinyi  viongozi wa dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi kwa waumini wenu kuhakikisha hamuonyeshi hisia za kuwa upande wa chama chochote cha kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegema chama au mgombea fulani” amesema Jaji Lubuva.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo , Askofu Philemon Phiri wa kanisa la EAGT-Mikocheni -A ameiasa Tume  hiyo  kusimama katika haki, uhuru na kuhakikisha wanatangaza washindi bila kuonyesha upendeleo  ili kuivusha nchi ikiwa  salama.

Mshiriki mwingine kutoka Kanisa la Moravian Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa amani ndiyo tunu kwa kila mwanadamu, hatutegemei vurugu wakati  huu wa uchaguzi maana amani inapotoweka wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini wao hivyo wao kama taasisi zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili tupate viongozi kwa amani

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutano na viongozi hao na wadau wengine ikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa kampeni hapo Jumamosi ijayo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Wednesday, August 19, 2015

MASSAGE THERAPY

MASSAGE THERAPY
Foreplan clinic is one of the biggest clinics in the world that uses different kinds of massage to treat different kinds of diseases. What is massage by the way, There are probably well over 100 types of massage, massage modalities, massage therapies and strokes. This is a basic overview of some of the most popular that can help your practice be a great success.
Types of Massage
ACUPRESSURE
 Acupressure technique utilizes pressure of the hand, fingers, elbow or other tools used to apply pressure to specific acupuncture points on the body. The pressing of these key areas on the body promotes better blood circulation and helps to relieve tension. Benefits from acupressure are many and range from relief of headaches to treating constipation. A therapist will use different pressure points depending on what the ailment or pain complaint might be. Many therapists might include a form of acupressure in any number of relaxation or therapeutic massages.
                       
 
ACUPUNCTURE
as the name implies, needles are placed into the skin along specific meridians and into Acupuncture points of the body. Acupuncture is very similar to Acupressure - difference being of course is that needles are used instead of fingers, hands, etc… This technique focuses on the “Qi” or energy flow of the body within the twelve main meridian pathways. This type of Traditional Chinese Medicine (TCM) is said to have many benefits in aiding treatment of ailments ranging from breathing difficulty to migraines to arthritis to name a few. Recent research continues to show positive results with treatment using Acupuncture.
     
AYURVEDA
 ayurveda is much more than a massage modality, but needs to be mentioned within this page of information because of the importance and history involved with Ayurveda. Ayurveda is an actual complete medical belief and philosophy developed in India (5000+ years ago) that is used to bring the mind and body to a deep inner peace creating harmony and life balance. Ayurvedic massage stems from this practice and takes into account the energies of the five elements of ether, air, fire, water and earth. The Ayurvedic physician then determines massage type and type of treatment combined with specific oils and herbs to get the most desirable healing results.

REFLEXOLOGY
reflexology can be used on feet, hands or ears. Specific areas on the feet, hands and ears correspond to certain parts of the body (internal glands and organs are included). The theory is that pressure applied in certain areas sends signals to the corresponding location, gland or organ through the nervous system helping to provide balance to the desired area. Stimulating these areas can be used to reduce pain, ease addiction, relieve stress and tension and improve nerve and blood circulation to name a few.
                                    
SPORTS MASSAGE
Sports massage is used as a preventive medicine for many athletes before, during and after sporting events. A combination of techniques such as Swedish massage, Shiatsu, Trigger point and Relaxation before an athletic event can prepare the athlete for increased performance. During events to keep the muscles loosened and warmed up to reduce injuries and after a hard workout to rid the body of stress, relieve fatigue and remove toxins and byproducts the body produces in strenuous activity. Massage can make the training and body building experience much more effective.

And those are some of the massages that Foreplan clinic use to help different individual. For more information please visit us at foreplan clinic Ilala Bungoni or contact use through 0762 400 400 or 0767 600 600.

Health Pregnancy Fact Sheet

  Michael

What do we mean by "healthy pregnancy"? A pregnancy that lasts the full nine months, A pregnancy that results in a healthy baby (or babies) weighing at least five and a half pounds who has no birth defects, A pregnancy in which the mother feels well the whole nine months other than the normal discomforts such as morning sickness.

What outcomes do we worry about for the baby? For the baby, the most common problem is low birth weight. A baby who is born weighing less than five and a half pounds is considered low birth weight. Low birth weight is the number one risk factor for death in the first year of life and for life-long health problems. It can be caused by being born too early, by growing too slowly, or some of both. Smoking by the mother is one of the main causes of poor growth, because it cuts down on the baby's supply of oxygen and food. Poor nutrition, birth defects, genetic conditions, mother's health problems such as high blood pressure, hazards in the environment including lead or tobacco smoke, and multiple births (twins, triplets, etc.) may also cause low birth weight. In many cases, the exact cause of low birth weight is not known.
What should pregnant women do?
It’s important to eat well-balanced meals and take prenatal vitamins during your pregnancy so that your developing baby can get all the essential nutrients it needs to grow strong. You should consume about 300 additional calories a day during this time.
What can a woman do to help her have a healthy pregnancy? The key to a healthy pregnancy is planning it in the first place. When pregnancies are planned, the mother-to-be can be in the best health possible and be ready for all the challenges of having a healthy baby and raising a family. Most people don't think about birth control as a way to have a healthy baby, but it plays a key role by helping women plan the best time to have a baby. When a woman is planning a pregnancy, she should be in the best health possible and should follow these guidelines: Take a multivitamin every day that has 400 mcg (0.4 mg) of folic acid. Folic acid is a B vitamin that helps prevent serious birth defects of the heart and brain. But it only helps if the mother takes it before pregnancy and in the first three months of pregnancy. Stop smoking. Get others at home and at work to stop smoking too to cut down on second-hand smoke. Stop drinking alcohol and/or using illegal drugs. Fetal Alcohol Syndrome is one of the most common birth defects. Every case is preventable by not drinking alcohol during pregnancy. Have a pre-pregnancy health check-up with a doctor, midwife, or nurse practitioner. Women with chronic health problems such as diabetes or high blood pressure and women who take medicines or herbs especially need pre-pregnancy care. Talk to your health care provider about the possible risk of lead poisoning. If lead gets into your body, it could harm you and your unborn baby.
What can a woman do after she gets pregnant to have a healthy pregnancy? Get prenatal care early. Go to all your regularly scheduled doctor appointments. Eat a well-balanced diet. Continue to take a multivitamin to be sure that mother and baby both get the nutrients they need. Gain enough weight, but not too much. Sign up for WIC, if you qualify. WIC provides extra food for pregnant and breastfeeding women and for infants and children. It also provides health education and support during pregnancy and breastfeeding. Get help with causes of stress, including family violence or work and school problems. There are sources of help in every community: schools, clinics, community centers, churches, and other organizations. Take a childbirth class to learn more about having a healthy birth and a healthy baby. Talk to your doctor or midwife if you believe you might be exposed to lead from:
paint chips or dust in apartments or houses built before 1978, working in a battery factory, re-finishing old furniture, or other jobs and hobbies working with lead, eating certain materials such as clay or dirt, some spices, foods and medicines from other countries, and using chipped or broken dishes to store food. Always wash your hands before making meals or eating. Pregnancy is a time of life when a women needs to rely on help from others. Your husband or partner, other family members or neighbors can: help around the house, help you prepare healthy foods, help you get to doctor appointments. Teens may need extra help sticking to good health habits.
Source: ForePlan Clinic

Chadema watangaza majina ya wagombea ubunge


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa orodha ya majina 138 ya wanachama walioteuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kugombea ubunge wa majimbo ya uchaguzi.

Orodha ya majina hayo ya wanachama walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo hayo, imesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kwa niaba ya Katibu Mkuu.
 
Taarifa imeeleza kuwa majimbo ambayo hayatakuwa kwenye orodha hiyo yatatolewa baada ya kukamilika kwa mashauriano ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
 
Katika mgawanyo wa UKAWA wa majimbo 253 Kati ya 265 ya kuwania ubunge, Chadema imeongoza kwa kupata majimbo 138 (54%), ikifuatiwa na CUF majimbo 99 (29% yakiwemo 49 ya Zanzibar), NCCR-Mageuzi majimbo 14 (5.5%) na NLD majimbo matatu (1.2%).
 
Ifuatayo ni orodha kamili ya majina ya wanachama wa Chadema walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo hayo.
 
Mara                        
  1. Rorya   STEVEN J OWAWA
  2. Tarime Mjini ESTHER N MATIKO
  3. Tarime Vijijini JOHN HECHE
  4. Musoma Vijijini ZAKARIA MBULA CHIRAGWILE
  5. Butiama        YUSUPH R KAZI
  6. Bunda Mjini  ESTHER BULAYA
  7. Mwibara  HARUN D CHIRIKO
  8. Musoma Mjini       VINCENT J NYERERE
  9. Bunda Vijijini  SULEIMAN DAUDI
Simiyu                      
  1. Bariadi        GODWIN SIMBA
  2. Maswa Magharibi ABDALA PATEL
  3. Maswa Mashariki SYLVESTER KASULUMBAYI
  4. Kisesa MASANJA MANANI
  5. Meatu          MESHACK OPULUKWA
  6. Itilima         MARTINE MAGILE
Shinyanga                
  1. Msalala             PAULO MALAIKA
  2. Kahama Mjini JAMES LEMBELI
  3. Kahama Vijijini (Ushetu) SIMON BUKAKIYE ISAYA
  4. Shinyanga Mjini PATROAS PASCHAL K
  5. Kishapu         FRED T MPENDAZOE
Mwanza                   
  1. Ukerewe JOSEPH MKUNDI
  2. Magu          KALWINZI NGONGOSEKE
  3. Nyamagana    EZEKIA D. WENJE
  4. Buchosa MARTINE KASWAHILI
  5. Sengerema HAMIS TABASAMU
  6. Ilemela         HIGHNESS KIWIA
  7. Misungwi LEONIDAS KONDELA
Geita                        
  1. Bukombe PROF. KULIKOYELA KAHIGI
  2. Busanda ALPHONCE C MAWAZO
  3. Nyang’wale GEORGE MABULA
  4. Chato          DR. BENEDICT LUKANIMA
  5. Mbogwe NICODEMUS H MAGANGA
Kagera                     
  1. Karagwe          PRINCE RWAZO
  2. Kyerwa          BENEDICT MTUNGIREHI
  3. Bukoba Mjini  WILFRED LWAKATARE
  4. Muleba Kaskazini  ANSBERT NGURUMO
  5. Muleba Kusini  ALISTIDES KASHASILA
  6. Biharamulo  DR. ANTHONY MBASSA
Mbeya                     
  1. Lupa         NJELU KASAKA
  2. Songwe          MPOKI MWANKUSYE
  3. Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI
  4. Kyela          ABRAHAM H MWANYAMAKI
  5. Rungwe         JOHN D MWAMBIGIJA
  6. Busokelo BONIPHACE A MWAMUKUSI
  7. Mbozi       PASCHAL HAONGA
  8. Momba        DAVID E SILINDE
  9. Mbeya Vijijini ADAM NZELA
  10. Tunduma FRANK MWAKAJOKA
  11. Vwawa FANUEL MKISI
Iringa                       
  1. Ismani         PATRICK OLE SOSOPI
  2. Kalenga        MUSSA L MDEDE
  3. Mufindi Kaskazini JUMANNE K MASONDA
  4. Iringa Mjini PETER MSIGWA
  5. Kilolo          BRIAN KIKOTI
  6. Mafinga Mjini WILLE MUNGAI
Njombe                    
  1. Njombe Kusini EMMANUEL MASONGA
  2. Lupembe (Njombe Kask) EDWIN E SWALE
  3. Wanging’ombe DISMAS A LUHWAGO
  4. Makete          JACKSON T MOGELA
  5. Ludewa           ATHROMEO MKINGA
  6. Makambako ORAPH MHEMA
Rukwa                     
  1. Nkasi Kusini ALFRED DANIEL SOTOKA
  2. Kwela          DANIEL NAFTAL NGOGO
  3. Nkasi Kaskazini KESSY SOUD
  4. Sumbawanga Mjini SADRICK MALILA
  5. Kalambo        VICTOR MATENI
Tanga                       
  1. Kilindi         JERADI K MREMA
  2. Muheza ERNEST MSINGWA
  3. Korogwe          AMANI H KIMEA
  4. Korogwe Vijijini EMMANUEL KIMEA
Kilimanjaro                       
  1. Rombo                   JOSEPH SELASIN
  2. Same Magharibi CHRISTOPHER S MBAJO
  3. Same Mashariki NAGENJWA KABOYOKA
  4. Moshi Mjini JAFARY P MICHAEL
  5. Hai          FREEMAN A MBOWE
  6. Siha         DR. GODWIN MOLLEL
Arusha                     
  1. Arumeru Mashariki JOSHUA NASSARI
  2. Arumeru Magharibi GIBSON MESIYEKI
  3. Arusha Mjini GODBLESS LEMA
  4. Longido        ONESMO OLE NANGOLE
  5. Monduli        JULIUS KALANGA
  6. Karatu         WILLE QAMBALO
  7. Ngorongoro ELIAS NGORISA
Manyara                  
  1. Simanjiro JAMES KINYASI OLE MILLYA
  2. Mbulu Vijijini MIKEL PETRO AWEDA
  3. Hanang          MAGOMA RASHID DERICK
  4. Babati Mjini PAULINE P GEKUL
  5. Babati Vijijini LAURENT SURUMBU TARRA
  6. Kiteto        KIDAWA ATHUMANI IYAVU
  7. Mbulu Mjini PAULO HERMAN SULLE
Dar es Salaam                  
  1. Ubungo        SAED KUBENEA
  2. Kawe        HALIMA JAMES MDEE
  3. Ukonga          MWITA MWIKWABE WAITARA
  4. Ilala         MUSLIM HASSANALI HEIDERALI
  5. Kibamba JOHN JOHN MNYIKA
Pwani                       
  1. Chalinze MATHAYO TM. TORONGEY
  2. Kibaha Mjini MICHAEL PAUL MTALY
  3. Kibaha Vijijini EDITHA BABBEIYA
Morogoro                
  1. Mikumi         JOSEPH HAULE
  2. Morogoro Kusini DAVID LUKAGINGIRA
  3. Kilombero PETER E LIJUALIKALI
  4. Mlimba        SUZAN L. KIWANGA
  5. Mvomero OSWALD MLAY
  6. Ulanga Magharibi ALPHONCE MBASSA
  7. Ulanga Mashariki PANCRAS KONGOLI
  8. Morogoro Mjini MARCOSSY ALBANIE
Dodoma                   
  1. Kongwa             ESAU NGOMBEI
  2. Dodoma Mjini SINGO BENSON KIGAILA
  3. Bahi         MATHIAS LYAMUNDA
  4. Chilonwa JOHN CHOGONGO
Singida                     
  1. Iramba Magharibi JESCA KISHOA
  2. Iramba Mash(Mkalama) OSCAR KAPALALE
  3. Singida kaskazini DAVID DJUMBE
  4. Singida Mashariki TUNDU A LISSU
  5. Singida Magharibi MARCO ALLUTE
  6. Manyoni Magharibi LUPAA DONALD
  7. Manyoni Mashariki ALLUTE EMMANUEL
Tabora                     
  1. Nzega Mjini CHARLES MABULA
  2. Igunga        NG’WIGULU KUBE
  3. Urambo         SAMWELI NTAKAMLENGA
  4. Ulyankulu DEUS KITAPANDYA NGERERE
  5. Sikonge       SAID NKUMBA
  6. Manonga ALLY KHALFANI NGUZO
Katavi                      
  1. Mpanda Mjini JONAS KALINDE
  2. Mpanda Vijijini MUSSA MASANJA
  3. Katavi          GEORGE SAMBWE
  4. Nsimbo GERALD KITABU
  5. Kavuu         LAURENT SENGA MANGWESHI
Kigoma                    
  1. Kigoma Kaskazini DR. YARED FUBUSA
  2. Kigoma Mjini          DANIEL LUMENYELA
Ruvuma                   
  1. Peramiho         ELASMO MWINGIRA
  2. Mbinga Magharibi/Nyasa CUTHBERT S. NGWATA
  3. Mbinga/Mbinga Vijijini EDWIN B AKITANDA
  4. Songea Mjini        JOSEPH FUIME
  5. Madaba EDSON MBOGORO

Monday, August 17, 2015

KILIMO BORA CHA MIHOGO

Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO
  1. Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
    • Naliendele
                 Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.


    • Kiroba
Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

  1. Mbinu bora za kilimo cha muhogo
    • Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
- Kufyeka shamba
- Kung’a na kuchoma visiki
- Kulima na kutengeneza matuta
·         Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
·         Upanadaji
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
-          Kulaza ardhini (Horizontal)
-          Kusimamisha wima (Vertcal)
-          Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
 Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.


·         Palizi:
-          Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
-          Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
-          Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
-          Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

·         Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

·         Usindikaji bora
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
-          Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
-          Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
-          Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji
-          Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
-          Kwa kutumia mashine aina ya chipper
-          Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

Matumizi ya Muhogo
-          Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
-          Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
-          Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.